

Rais Samia Suluhu Hassan jana Mei 8,2025 ametuma salamu za pongezi kwa Papa mpya akimtakia kila laheri.
Katika kusara zake za mitandao ya kijamii aliandika:
Habemus Papam!
Pongezi za dhati kwa Kardinali Robert Francis Prevost, Papa Leo XIV kwa kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani.
Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninakutakia kila la kheri katika utumishi wako kwa Kanisa na Dunia kwa ujumla.
Mwenyezi Mungu akusimamie na kukuongoza.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!