Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MAGAZETI ya Leo Jumatano 07 May 2025

  • 58
Scroll Down To Discover

MAGAZETI ya Leo Jumatano 07 May 2025

Taarifa za uhakika ni kuwa Simba iko katika mchakato wa kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Azam Fc, Feisal Salum ‘Fei Toto’

Inaelezwa kuwa juzi Rais wa heshima wa Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ alifanya mazungumzo na Wawakilishi wa Fei Toto ambapo kimsingi ‘tajiri amempa Fei ofa nono ya mshahara na dau la usajili

Hatua iliyobaki ni kukamilisha mazungumzo na Azam Fc ambayo bado inamkataba wa mwaka mmoja na Fei Toto ambaye alijiunga na timu hiyo misimu miwili iliyopita akitokea Yanga

Simba ina uhakika wa kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao na malengo ni kufanya vyema kama walivyofanya msimu huu katika michuano ya kombe la Shirikisho Simba ikitinga fainali ambapo itacheza na RS Berkane

Fei Toto amekuwa ‘injini’ ya Azam Fc katika misimu miwili akifunga mabao 23 na kutoa pasi 21 za mabao

Jean Charles Ahoua ndiye tegemeo katika la kiungo cha ushambuliaji cha Simba lakini ni wazi imeonekana eneo hilo linahitaji kuongezewa nguvu, Fei Toto ndiye kiungo bora wa ushambuliaji kwa sasa katika ligi kuu ya Tanzania.



Prev Post Makalla: Mafaniko Tunayojivynia ni Utekelezaji wa Malengo ya Kuundwa Kwa CCM
Next Post Rais Dkt.Samia afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali -Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook