Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makalla: Mafaniko Tunayojivynia ni Utekelezaji wa Malengo ya Kuundwa Kwa CCM

  • 46
Scroll Down To Discover

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema mafanikio wanayojivunia ni utekelezaji wa malengo ya kuundwa kwa chama chao tangu hapo Februari 5,1977.

Makalla ameeleza hayo leo Mei 6,2025 wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mbembe Songo katika Jimbo la Morogoro Mjini mkoani Morogoro ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani humo.

Makalla amesema kuungana kwa vyama hivyo viwili iliwekwa misingi ya kuunda chama imara na kikubwa kitakacholeta mageuzi na mapinduzi katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi na misingi hiyo wanaitekeleza hadi sasa.

“Tunawakumbusha kwamba mwaka huu CCM ilitimiza miaka 48 historia inaeleza wakati vyama hivi vikiungana TANU na ASP walipokaa azimio, nanukuu kwamba itakapofika Februari 5 vyama vyetu tutavivunja na kuunda chama kikubwa,” amesema Makalla.

Ameongeza: “Chama kitakacholeta mageuzi na mapinduzi ya kijamii na kiuchumi na mapinduzi hayo yanatekelezwa toka kuundwa kwa CCM hatujaacha mpaka sasa”.

Makalla alisema maendeleo yanafanyika na mafanikio yanayoelezwa ni kutokana na misingi hiyo na imani ya wananchi kwa CCM inatikana na mambo yaliyofanyika katika nyanja ya elimu, afya.

Aidha, amesema Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdul-Azizi Abood ameelza mambo yaliyofanywa katika jimbo hilo na kutokana na mambo hayo wananchi wataendelea kuwa na imani kwa CCM.

Katika hatua nyingine Makalla amempongeza Abood kwa kuwa mkweli kwani ameelzea hatua kwa hatua na ameweka wazi changamoto zilizopo pamoja na kuwa na mafanikio na kuwa mkweli ni jambo zuri katika uongozi.



Prev Post Mpenzi Wangu Alioa Mwanamke Mwingine Zikiwa Zimebaki Siku 2 Kabla ya Harusi Yetu
Next Post MAGAZETI ya Leo Jumatano 07 May 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook