Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Afrika Mashariki yapanga kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta Tanga

  • 9
Scroll Down To Discover

Rais wa Kenya, William Ruto amesema nchi za Afrika Mashariki zinajadili mpango wa kujenga kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta katika bandari ya Tanga, kikifanana na kile cha Aliko Dangote cha nchini Nigeria.

Ruto amesema hayo kwenye mkutano wa ‘Africa We Build Summit 2026’ jijini Nairobi ambapo amebainisha kuwa kiwanda hicho kitahudumia nchi kadhaa kwa kutumia mafuta ghafi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Sudan Kusini na Uganda.

Kwa upande wake Dangote ambaye pia amehudhuria mkutano huo amesema yuko tayari kujenga kiwanda kama chake chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku, ikiwa serikali za nchi hizo zitatoa ushirikiano.

“Ahadi yangu hapa ni kwamba ikiwa tutakubaliana na serikali tatu au nne hapa kuhusu kiwanda cha kusafisha mafuta, tutahakikisha kuwa kiwanda cha kusafisha kinajengwa ndani ya miaka minne au mitano ijayo,” amesema Dangote.

The post Afrika Mashariki yapanga kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta Tanga appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO APRILI 23, 2026
Next Post NMB ilivyosaidia serikali kukusanya zaidi ya TZS trilioni 9.8
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook