Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

KUELEKA MUUNGANO CUP LEO….AKILI YA PEDRO HUKO YANGA NI MOJA TU AISEEE….

  • 6
Scroll Down To Discover

YANGA imetua kisiwani Zanzibar tayari kwa kutetea Kombe la Muungano, lakini ilipogusa ardhi ya hapa tu kuna kauli kaitoa kocha wa timu hiyo, Pedro Goncalves ambayo itashtua wapinzani.

Ikitua jana asubuhi, Pedro amesema kikosi chake kipo tayari kwa mechi tatu ngumu zitakazowasaidia kutetea ubingwa, akisema wachezaji pekee ambao hawakusafiri na timu hiyo ni wale ambao hawataweza kucheza tena msimu huu.

Pedro amesema kila mchezaji ana nafasi kwenye mashindano ambayo Yanga inashiriki ambapo wameshajua namna gani wataanza mechi hizo leo itakapocheza dhidi ya Mwembe Makumbi City saa 1:15 usiku.

Yanga inashikilia taji hilo ililolichukua msimu uliopita baada ya kuichapa JKU ya hapa Zanzibar kwa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Maxi Nzengeli, mechi iliyochezwa Mei Mosi 2025 pale Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba.

“Tumefika hapa, kama ilivyo kawaida hii ni timu ambayo wakati wote inahitaji mafanikio, tumekuja kama bingwa mtetezi, tunataka kuendeleza yale ambayo tuliyafanya msimu uliopita,” amesema Pedro ambaye atashiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo huku akiwa na kumbukumbu ya kubeba Kombe la Mapinduzi 2026 kisiwani hapa.

“Nilikuwa hapa wakati wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi, najua namna ilivyo ngumu kushinda dhidi ya timu za hapa, hatuwezi kuchukulia rahisi timu ya Mwembe Makumbi.

“Tumekuja na timu kamili, wachezaji ambao tumewaacha nyuma ni wale ambao tunaona sio rahisi sana kucheza msimu huu lakini wengine wote wako hapa tutakuwa na mechi tatu mpaka kufika fainali,” amesema.

Aidha Pedro amesema Yanga haiwezi kuogopa mpinzani yeyote ambapo kikosi chake kitacheza kwa kiwango kikubwa kulingana na ubora wa mpinzani aliye mbele yao wakitumia ubora wao.

“Hakuna nafasi ya kuhofia timu yoyote unapokuwa unafanya kazi na timu kama hii ya Yanga, tuna wachezaji waliokomaa, wanajua namna ya kucheza mechi za presha, tutawaheshimu wapinzani ambao tutakutana nao, kila timu tutakuwa na mpango wa kucheza nayo,” amesema.

Mchezo wa mwisho kwa Pedro kushinda kisiwani hapa ni pale alipoichapa Azam kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026, iliyopigwa pale Gombani, Januari 13, 2026.

The post KUELEKA MUUNGANO CUP LEO….AKILI YA PEDRO HUKO YANGA NI MOJA TU AISEEE…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KWA HILI LA MANARA…HAPANA KWA KWELI….NI ZAIDI YA USALITI…
Next Post MAJABU YA HARY KANE …BAYEN WAKIBEBA UBINGWA WA 35 BUNDESLIGA….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook