Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Stanbic yatajwa Benki Bora ya Kimataifa kwa Wateja Maalum kwa mwaka wa pili mfululizo

  • 9
Scroll Down To Discover


Benki ya Stanbic imepata tuzo tatu za kimataifa ambazo ni Benki Bora ya Kimataifa kwa Wateja Maalum, Benki Bora kwa Kizazi Kijacho, na Benki Bora kwa Huduma kwa Wateja, zikionesha mchango wake katika kusaidia wateja wa Tanzania kujenga, kukuza na kulinda ukwasi wao kwa mtazamo wa muda mrefu na vizazi vijavyo. 

Tuzo hizo zilitolewa na Jarida la Euromoney baada ya tathmini ya kina iliyofanywa na jopo huru la wataalamu wa sekta ya kibenki, na zilitangazwa katika hafla ya Euromoney Private Banking Awards 2026 iliyofanyika jijini London mwishoni mwa wiki. 


Utambuzi huu unakuja wakati uchumi wa Tanzania unaendelea kukua, ukiwa na makadirio ya ukuaji wa kati ya asilimia 5 hadi 6 kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, sambamba na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi na uwekezaji. Hali hii imechochea ukuaji wa ukwasi, hasa kwa wajasiriamali na biashara za kifamilia.  Tuzo hizi tatu zinaakisi maeneo muhimu yanayoongoza mabadiliko haya.

Tuzo ya Benki Bora ya Kimataifa kwa Wateja Maalum inaonesha uwezo wa Stanbic kuwaunganisha wateja wake na masoko ya kimataifa pamoja na fursa za uwekezaji, hivyo kuwawezesha kukuza ukwasi wao ndani ya mipaka ya nchi. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa benki kupata utambuzi huu, jambo linaloonesha ushawishi wake katika kutoa suluhisho za kifedha za kimataifa. 

Tuzo ya Benki Bora kwa Kizazi Kijacho inaangazia mpango wa kuwaandaa warithi na vijana kusimamia mali kwa uwajibikaji, hasa wakati biashara nyingi za kifamilia zinaanza kupokelewa na kizazi kipya. 
Tuzo ya Benki Bora kwa Huduma kwa Wateja inaonesha umuhimu wa mahusiano ya muda mrefu, na ushauri unaolengwa mahususi kwa kila mteja katika kumsaidia kufanya maamuzi ya kifedha yenye uzito kwa kipindi cha muda mrefu. 


Akizungumzia mafanikio hayo, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira, alisema tuzo hizo zinaonesha mabadiliko mapana katika namna mali zinavyoundwa na kudumishwa nchini.

“Kwa Tanzania, mali mara nyingi hazibaki kwa mtu mmoja pekee. Zinahudumia familia, zinaendeleza biashara na zinachangia jamii. Kadri mali zinavyozidi kuongezeka, ndivyo umuhimu wa kuzipanga, kuzilinda na kuhakikisha zinarithishwa kwa ufanisi kwa vizazi vijavyo unavyoongezeka. Tuzo hizi zinaakisi kazi tunayoifanya kusaidia wateja wetu katika safari hiyo,” alisema. 

Licha ya ukuaji mzuri wa uchumi, upatikaniji wa huduma za kifedha nchini bado ni mdogo ukilinganisha na masoko yaliyoendelea, ambapo mikopo kwa sekta binafsi bado inachangia sehemu ndogo ya pato la taifa kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania. Hali hii inaonesha fursa kubwa ya kuimarisha suluhisho za kifedha zilizopangiliwa zaidi, zikiwemo ushauri wa uwekezaji, mipango ya mali na usimamizi wa urithi. 

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Wateja Maalum wa Benki ya Stanbic, Omari Mtiga, alisema huduma kwa wateja maalum sasa zinaelekezwa zaidi katika kujenga ushirikiano wa muda mrefu na mwendelezo wa kifedha.

“Jukumu letu ni kuelewa safari kamili ya mteja, biashara zake, familia yake na malengo yake ya baadaye. Tunafanya kazi nao kuhakikisha mali zao si tu zinahifadhiwa, bali pia zinarithishwa kwa mpangilio unaoleta uendelevu,” alisema. 

Kwa vitendo, mabadiliko haya yanaonekana katika mazungumzo kati ya wateja na benki zao, ambapo sasa kuna msisitizo mkubwa zaidi kwenye utawala bora wa kifedha, uelewa wa masuala ya fedha, na maandalizi ya kizazi kijacho kuchukua nafasi za uongozi. 

Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Maalum Stanbic, Beatrice Kisoka, alisema wateja wengi sasa wanaangalia zaidi ya mafanikio ya sasa. “Wateja wengi wanazingatia maana halisi ya mali zao kwa familia na vizazi vijavyo. Wanataka kuona mwendelezo, uthabiti na athari ya muda mrefu, na hilo linahitaji mwongozo pamoja na mipango iliyopangiliwa vizuri,” alisema. 

Mbali na ushauri wa ndani ya nchi, Benki ya Stanbic inaunganisha wateja wake na masoko ya kimataifa pamoja na elimu ya uwekezaji, ili kuwawezesha kupanua uwekezaji wao na kuwekeza katika maeneo tofauti tofauti.

Tuzo za Euromoney zinaimarisha nafasi ya Stanbic kama mshirika wa karibu kwa wateja wanaotaka kujenga, kukuza na kulinda mali zao kwa namna inayozalisha thamani ya kudumu zaidi ya mafanikio ya mtu mmoja. 

Aidha, tuzo hizi zinakuja kipindi ambapo Benki ya Stanbic imetajwa kuwa Benki Bora nchini Tanzania kwa mwaka 2025 na jarida la The Banker, jambo linaloonesha uthabiti wa benki katika shughuli zake zote. 

The post Stanbic yatajwa Benki Bora ya Kimataifa kwa Wateja Maalum kwa mwaka wa pili mfululizo appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Tanzania Breweries PLC Yaendeleza Mafanikio Kupitia Mbio za Kilimanjaro Marathon 2026
Next Post STANBIC YAWEZESHA BIASHARA ZA BILIONI 200 KATI YA TANZANIA NA CHINA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook