Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Shule Ya Msingi Kiromo Yakarabatiwa Kwa Ufadhili Wa Airtel

  • 11
Scroll Down To Discover

Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, ametembelea Shule ya Msingi Kiromo kukagua maendeleo ya mradi wa ukarabati unaofadhiliwa na kampuni hiyo, wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na walimu.

Katika ziara hiyo, viongozi wa Airtel walipata taarifa ya hatua za ukarabati wa miundombinu ya shule, unaolenga kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora na salama ya kusomea.

Akizungumza wakati wa ziara, Mkuu wa Sheria na Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano, amesema kampuni itaendelea kusaidia sekta ya elimu kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii.

Amesema pamoja na ukarabati unaoendelea, Airtel itatoa meza 250 mpya ili kupunguza changamoto ya uhaba wa samani madarasani na kuboresha mazingira ya kujifunzia.

Uongozi wa Shule ya Msingi Kiromo umeishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo, ukieleza kuwa maboresho ya miundombinu na upatikanaji wa vifaa yataongeza ari ya wanafunzi kusoma na kufikia malengo yao ya kielimu.

Stori Na Richard Bukosi, GPL

The post Shule Ya Msingi Kiromo Yakarabatiwa Kwa Ufadhili Wa Airtel appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Amkabidhi Msaada wa Shilingi Milioni 10 Mzee Zahir Zorro
Next Post Video: ‘House Girl’ Afikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma Za Kujaribu Kuua Kichanga
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook