Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Amkabidhi Msaada wa Shilingi Milioni 10 Mzee Zahir Zorro

  • 13
Scroll Down To Discover

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma Akimkabidhi Shilingi Milioni 10 Mzee Zahir Ally Zorro

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, Machi 8, 2026, amemtembelea na kumjulia hali mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Zahir Ally Zorro, nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo, Mwinjuma alimkabidhi Zorro kiasi cha shilingi milioni 10 taslimu ikiwa ni salamu za pole na faraja kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimtakia apone haraka.

Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Zahir Ally Zorro Akiwa Kitandani, Nyumbani Kwake

Akizungumza baada ya kumjulia hali, Mwinjuma alisema Serikali inaendelea kuthamini mchango wa wasanii wakongwe katika kukuza sanaa na utamaduni wa Tanzania, akisisitiza kuwa ni hazina muhimu ya taifa inayostahili kuenziwa na kupewa faraja wanapopata changamoto.

Kwa upande wake, Zahir Ally Zorro aliishukuru Serikali na Rais Samia kwa upendo na kujali hali yake, akisema msaada huo ni faraja kubwa kwake na kwa familia yake katika kipindi anachopitia.

 

The post Rais Samia Amkabidhi Msaada wa Shilingi Milioni 10 Mzee Zahir Zorro appeared first on Global Publishers.



Prev Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO MACHI 08, 2026
Next Post Shule Ya Msingi Kiromo Yakarabatiwa Kwa Ufadhili Wa Airtel
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook