Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mlipuko Mkubwa Watikisa Uwanja wa Ndege wa Dubai Baada ya Drone Kuanguka

  • 15
Scroll Down To Discover

Taharuki kubwa imeripotiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai kufuatia mlipuko mkubwa unaodaiwa kusababishwa na drone ya kujitoa mhanga inayodaiwa kutoka Iran. Tukio hilo limetokea  leo Jumamosi karibu na maeneo ya vituo vya abiria katika uwanja huo wenye shughuli nyingi zaidi katika jiji la Dubai.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mlipuko huo ulisababisha taharuki kubwa katika uwanja huo wa ndege, ambapo abiria walionekana wakikimbia kutafuta usalama huku baadhi ya maeneo ya uwanja huo yakianza kuhamishwa watu haraka.

Mamlaka za usalama zilichukua hatua za haraka kwa kusitisha safari za ndege kwa muda na kuanza operesheni za dharura wakati uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.

Hadi sasa, mamlaka hazijatoa taarifa rasmi kuhusu idadi ya watu waliojeruhiwa au kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mlipuko huo. Uchunguzi unaendelea ili kubaini iwapo drone hiyo ilihusishwa na shambulio la makusudi au tukio jingine la kiusalama.

MAREKANI YAIDHINISHA MAUZO ya SILAHA za DOLA MILIONI 151+ kwa ISRAEL – YAPO MAKOMBORA 12,000 📍ISRAEL

The post Mlipuko Mkubwa Watikisa Uwanja wa Ndege wa Dubai Baada ya Drone Kuanguka appeared first on Global Publishers.



Prev Post Rais Samia Ashiriki Mazungumzo na Viongozi wa EAC Arusha
Next Post Mkuu wa Quds Force wa Iran Adaiwa Kunyongwa Akituhumiwa Kuwa Jasusi wa Israel na Marekani
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook