Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wachungaji Wamwombea Rais Trump Ikulu ya Marekani

  • 14
Scroll Down To Discover

Donald Trump amefanyiwa maombi maalum na wachungaji kadhaa katika ofisi ya Oval Office, wakimuombea hekima, uimara na uwezo wa kuliongoza taifa la Marekani.

Tukio hilo lilifanyika jana ambapo wachungaji hao walikusanyika ndani ya ofisi hiyo na kumzunguka rais huyo huku wakimuombea kwa pamoja. Baadhi yao walimwekea mikono wakati wengine wakinyanyua mikono yao kama ishara ya baraka na maombi.

Katika maombi hayo, mmoja wa wachungaji alisikika akisema:
“Bwana mpe uimara anaouhitaji ili aweze kuliongoza taifa letu kubwa.”

Maombi hayo yalilenga kumuombea Rais Trump apate hekima, nguvu na uongozi thabiti katika kuongoza nchi hiyo wakati wa changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa hilo.

Tukio hilo limeibua mjadala katika mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watu wakiliona kama ishara ya imani na wengine wakijadili nafasi ya dini katika uongozi wa kisiasa nchini Marekani.

The post Wachungaji Wamwombea Rais Trump Ikulu ya Marekani appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Mkuu Mwigulu Awasili Arusha Kuzindua Miradi ya Kilimo na Kuzungumza na Wananchi
Next Post Takwimu za Siku 6 za Vita ya Iran na Mustakabali wa Amani Mashariki ya Kati
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook