Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Naibu Waziri Hamad Afika Kwenye Shamba la Kuku Kisarawe Linalozalisha Kuku Milioni 6

  • 17
Scroll Down To Discover

Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Zanzibar Dkt. Salum Soud Hamed

Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Dkt. Salum Soud Hamed, amefanya ziara maalum wilayani Kisarawe akiongozana na Kamati ya Utalii na Biashara, kutembelea shamba la kisasa la uzalishaji wa kuku wa mayai linalomilikiwa na kampuni ya @afi_green

Ziara hiyo imelenga kujifunza na kujionea fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na ufugaji, hususani ufugaji wa kuku wa mayai, kama njia ya kuongeza ajira na kukuza uchumi. Dkt. Hamed ameonesha nia ya kuwakaribisha wawekezaji hao Zanzibar ili kuwekeza na kutoa elimu kwa wananchi, hatua itakayochochea ajira kwa vijana.

Shamba la Kuku wa Mayai Kisarawe Linalozalisha Vifaranga Milioni 6 kwa Mwaka.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fatma Mandoba, amewapongeza Afi Green kwa kuwaajiri wazawa wa Kisarawe na kuwataka vijana wa Zanzibar kutotegemea sekta ya utalii pekee, bali kuchangamkia fursa za ufugaji wa kuku wa mayai zenye tija kubwa kiuchumi.

Katika shamba hilo, zaidi ya kuku wazazi 50,000 wanatunzwa, wakizalisha vifaranga kati ya 500,000 na 600,000 kila mwezi, sawa na wastani wa vifaranga milioni sita kwa mwaka.

The post Naibu Waziri Hamad Afika Kwenye Shamba la Kuku Kisarawe Linalozalisha Kuku Milioni 6 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Dkt. Migiro Aongoza Kikao Cha Bodi ya Wadhamini Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere
Next Post Video: Marekani na Israel Watangaza Mpango wa Kuchukua Udhibiti wa Anga ya Iran
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook