KOCHA wa Yanga SC, Pedro Goncalves, amekiri kuwa timu yake ilizidiwa katika dakika za mwanzo za mechi ya Kariakoo Derby, kutokana na kasi kubwa iliyowakilishwa na wapinzani wao, Simba SC.
Akizungumza baada ya mechi jana iliyochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Pedro alisema kwamba presha na nguvu za Simba mwanzoni zililazimisha wachezaji wake kuchukua tahadhari kabla ya kuingia vizuri kwenye mpango wao wa mchezo.
“Tulihitaji muda wa kuzoea, tumezoea kucheza na timu zinazokabia katikati, leo ilikuwa tofauti.
Namna Simba walivyobadilisha mbinu zao na kuanza kwa mashambulizi ya kasi kutoka pembeni pamoja na mipira mirefu ya kushtukiza, ilikuwa changamoto kubwa kwetu,” amesema Goncalves.
Kocha huyo ameeleza kuwa benchi la ufundi la Yanga lilikua tayari na lilijua jinsi ya kurekebisha hali.
“Lakini tulijua cha kufanya. Nilifanyia timu marekebisho ya kimkakati ambayo yaliisaidia kutulia, kumiliki mpira na kuanza kucheza kwa utaratibu wetu wa kawaida,” amesema.
Kadri dakika zilivyokuwa zikipita, Yanga walionekana kuimarika zaidi, wakiweza kurejesha nidhamu ya mchezo na kuanza kutengeneza nafasi zao.
Hii inaonyesha kwamba licha ya changamoto za mwanzo, timu ina uwezo wa kurekebisha mbinu zake na kuendelea kushindana kwa kiwango cha juu.
The post YANGA YAZIDIWA MWANZO, PEDRO AELEZA CHANGAMOTO appeared first on Soka La Bongo.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!