Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei ameuawa, televisheni ya serikali Yathibitisha

  • 12
Scroll Down To Discover

Taarifa kutoka Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran pamoja na vyombo kadhaa vya habari vya serikali vimethibitisha kifo cha Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, aliyekuwa na umri wa miaka 86.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Khamenei alifariki kufuatia mashambulizi ya pamoja yaliyoripotiwa kufanywa na Israel katika maeneo mbalimbali nchini Iran.

Hata hivyo, maelezo rasmi kuhusu mazingira halisi ya kifo chake hayajawekwa wazi, wala haijatajwa wazi ni nani atakayechukua nafasi yake katika uongozi wa juu wa nchi hiyo.

Kauli ya Rais wa Marekani Rais wa Marekani, Donald Trump, saa chache kabla ya uthibitisho huo, alieleza kuwa Kiongozi Mkuu huyo aliuawa katika operesheni maalum iliyolenga miundombinu muhimu ya Iran.

Kauli hiyo imeongeza taharuki kimataifa, huku wachambuzi wa siasa wakitabiri mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

Vyombo vya habari vya serikali pia vimeripoti kuwa baadhi ya wanafamilia wa Khamenei waliuawa katika mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa Fars News Agency, shirika la habari linalohusishwa na Kikosi cha Revolutionary Guard, binti wa Khamenei, mkwe wake na mjukuu wake ni miongoni mwa waliopoteza maisha. Ripoti nyingine zinaeleza kuwa mmoja wa mabinti zake pia aliuawa, ingawa taarifa hizo bado hazijathibitishwa kwa kina.

The post Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei ameuawa, televisheni ya serikali Yathibitisha appeared first on Global Publishers.



Prev Post Video: Maafisa 40 wa Iran Wauawa katika Mashambulizi ya Israel na Marekani
Next Post Nafasi za Kazi: Site Foreman Wenye Uzoefu wa Miaka 2 Wahitajika Haraka
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook