Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Iran Yatoa Onyo Kali kwa Marekani Kuhusu Mashambulizi na Mazungumzo ya Nyuklia

  • 14
Scroll Down To Discover

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa onyo kali kwa Marekani kuwa nchi yake itajibu mashambulizi yoyote ya kijeshi kwa kupiga kambi za Marekani zilizopo Mashariki ya Kati, huku akisisitiza kuwa Iran ina haki ya kuendelea na urutubishaji wa madini ya Urani.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS cha Marekani, Jumapili, Araghchi amebainisha kuwa ingawa Iran haitaki vita, haitasita kulinda mamlaka yake. Alieleza kuwa kwa sababu makombora yao hayawezi kufika moja kwa moja kwenye ardhi ya Marekani, shabaha yao kuu itakuwa kambi za kijeshi za Marekani katika ukanda huo, kama ilivyotokea mwaka jana katika kambi ya Al-Udeid nchini Qatar.

Pamoja na lugha hiyo ya kijeshi, Araghchi ametoa matumaini ya kupatikana kwa suluhu ya kidiplomasia katika duru ijayo ya mazungumzo inayotarajiwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi, Alhamisi ijayo.

“Ninaamini bado kuna nafasi nzuri ya kupata suluhu ya kidiplomasia ambayo inategemea mchezo wa pande zote kushinda (win-win). Tunafanya kazi katika vipengele vya mkataba na rasimu ya maandishi inakaribia kukamilika,” alisema Araghchi.

Changamoto kubwa katika mazungumzo hayo inabaki kuwa msimamo wa Iran kuhusu nishati ya nyuklia. Araghchi amesisitiza kuwa kama nchi huru, Iran ina haki ya kuamua yenyewe kuhusu urutubishaji wa Urani kwa matumizi ya kiraia, jambo ambalo Marekani imekuwa ikilipinga vikali kwa hofu ya kutengenezwa kwa silaha za nyuklia.

Stori na Elvan Stambuli, Global Digital

The post Iran Yatoa Onyo Kali kwa Marekani Kuhusu Mashambulizi na Mazungumzo ya Nyuklia appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mfanyakazi wa nyumbani, raia wa Uganda, kunyongwa Syria, katika Dira ya Dunia TV
Next Post Chalamila Asaini Kitabu Cha Maombolezo Kufuatia Kifo Cha Cardinali Pengo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook