Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aongoza Zoezi la Kutoa Huduma za Kisheria Kwa Wananchi

  • 22
Scroll Down To Discover

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amewaongoza Mawakili wa Serikali kutoa huduma za ushauri wa Kisheria kwa wananchi wakati wa Kliniki ya Sheria bila malipo iliyozinduliwa tarehe 16 Februari, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Johari amemuhudumia mwananchi aliyekuja kupata huduma ya ushauri wa kisheria ambapo alimsikiliza na kumuhudumia Bi. Sarah Mohamed aliyewasilisha malalamiko yake kuhusiana changamoto ya mirathi inayomkabili.

*“Tumeyapokea malalamiko yako na mimi pamoja na timu tutayafanyia kazi kwa haraka ili kuweza kutatua changamoto inayokukabili”.* Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Katika zoezi hilo la kutoa huduma kwa wananchi Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliambatana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainab A. Katimba.

Timu ya Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepiga kambi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kutoa huduma mbalimbali za kisheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 hadi 22 Februari, 2026.

The post Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aongoza Zoezi la Kutoa Huduma za Kisheria Kwa Wananchi appeared first on Global Publishers.



Prev Post Kenya na Ghana kuchunguza Mrusi kuhusu za siri za wanawake. Katika Dira ya Dunia TV
Next Post RC Chalamila Azindua Kliniki ya Sheria Jijini Dar es Salaam
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook