Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Mwigulu Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi Wa Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Ya Tanga

  • 20
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 15, 2026 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Tanga ambayo hadi kukamilika kwake kutagharimu zaidi cha shilingi bilioni 12

Chuo hicho kinachojengwa katika kata ya Gombero, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, unatekelezwa kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi” (“Higher Education for Economic Transformation” – HEET”)

Miradi inayoendelea kutekelezwa kupitia mpango huo ni Ujenzi wa Jengo la Taaluma lenye jumla ya madarasa 6, Maktaba ndogo, Ukumbi wa mihadhara, maabara mbili zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja, pamoja na ofisi 36 zitakazohudumia wafanyakazi 72.

Aidha majengo mengine ni Hosteli 2 za wanafunzi, Bwalo la Chakula, Kituo cha afya kitakachohudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa vijiji vilivyopo jirani na Chuo, Nyumba 4 za Wafanyakazi, Mfumo ya majitaka na dampo la kuhifadhia taka ngumu pamoja na Tenki la kuhifadhi Maji Safi la ujazo wa lita laki 4.

Hadi kufikia Februari 13, 2026 ujenzi wa kampasi hiyo ulikuwa umefikia asilimia 82

The post Dkt. Mwigulu Aweka Jiwe La Msingi Ujenzi Wa Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Ya Tanga appeared first on Global Publishers.



Prev Post TRA Yaanza Kutekeleza Maagizo ya Rais Samia Karatu
Next Post Rais Dkt. Samia Aondoka Addis Ababa Baada ya Kushiriki Mkutano wa AU
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook