Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais wa CAF Awasili Tanzania Kuhudhuria Mkutano Muhimu wa Soka

  • 21
Scroll Down To Discover

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amewasili rasmi nchini Tanzania asubuhi ya leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kamati Tendaji ya Shirikisho hilo.

Mutsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, Terminal 1, jijini Dar es Salaam.

Dkt. Motsepe ataongoza mkutano huo unaotarajiwa kufanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.

Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu.

Kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni ishara ya nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.

The post Rais wa CAF Awasili Tanzania Kuhudhuria Mkutano Muhimu wa Soka appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Mkuu Mwigulu Akagua na Kufungua Jengo la ICU Handeni
Next Post Mwanasheria Mkuu wa Serikali “Tunasogeza Huduma za Kisheria Karibu Zaidi na Wananchi”
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook