HESABU za kufuzu bado ni ngumu kwa Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika, hali inayowalazimu kuangalia zaidi ya mechi yao wenyewe.
Hii ni baada ya Yanga kuumiza kichwa wakijikuta wakiombea AS FAR Rabat kupoteza mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly ili wao wawe na nafasi ya kutinga robo fainali.
Wakati wakiomba matokeo mazuri kutoka kwa Al Ahly, Yanga pia ina kazi kubwa ya kuhakikisha wanashinda mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya JS Kabylie.
Mchezo huo utapigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, ambapo matarajio ni makubwa kwa Wananchi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, klabu hiyo bado ina matumaini makubwa ya kufuzu na anaamini Yanga inaweza kuwa timu pekee ya Tanzania itakayofika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Kamwe amesema Yanga wana imani ya kushinda mechi yao dhidi ya JS Kabylie, huku wakifuatilia kwa karibu pia matokeo ya mchezo kati ya Al Ahly na AS FAR Rabat, kuwa mechi hizo mbili zina umuhimu mkubwa katika hatima ya kufuzu kwao.
“Tunatambua ugumu wa mechi yetu, lakini pia tunajua kuna mchezo mwingine ambao matokeo yake yanatuhusu moja kwa moja. Suala la kwenda robo fainali bado lipo mikononi mwetu,” amesema Kamwe.
Ameongeza kuwa Yanga inapokuwa na dhamira ya kweli, huwa haishindwi, na anaamini Jumapili hii watapambana kwa nguvu zote ili kuhakikisha wanakuwa timu pekee itakayoiwakilisha Tanzania katika hatua za juu za mashindano ya kimataifa.
The post ROBO FAINALI BADO HAI, YANGA WASHIKA MAWILI appeared first on Soka La Bongo.






Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!