Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

MSIMBAZI MOTO MOTO SIMBA YAITAKA KMC KUREJEA

  • 24
Scroll Down To Discover

KIKOSI cha Simba kinaingia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC kikiwa chini ya presha kubwa ya kurejesha makali yake, hasa ikizingatiwa nafasi ya saba wanayoshika kwa sasa kwenye msimamo wa ligi.

Hali hiyo imechangiwa na uwepo wa viporo vingi vinavyolazimisha Wekundu wa Msimbazi kutafuta matokeo chanya kwa haraka ili kuendelea kuwania ubingwa.

Mashabiki wa Simba wanatarajia kuona mwitikio wa haraka kutoka kwa kikosi chao, hususan baada ya changamoto walizokutana nazo kwenye michuano ya kimataifa. Kwa sasa, kila mchezo wa ligi unachukuliwa kama fainali, kwani kupoteza pointi yoyote kunaweza kuathiri mwelekeo wao wa msimu huu.

Mchezo dhidi ya KMC unatajwa kuwa mtihani wa kwanza kwa Simba kuthibitisha kama kweli wameanza kurejea kwenye ubora wao wa kawaida au bado wanaendelea kusaka uthabiti ndani ya kikosi.

Morali ya kikosi cha Simba inaelezwa kuwa juu kuelekea mchezo huo, hasa baada ya kuonyesha kiwango kizuri wakiwa ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Petro Atletico ya Angola, ambapo walifanikiwa kutoka sare ya bao 1-1. Matokeo hayo yameongeza imani na ari kwa Wekundu wa Msimbazi licha ya changamoto walizokutana nazo kwenye mchezo huo.

Zaidi ya hilo, wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili wameonyesha dalili nzuri za ubora wao, jambo lililowapa matumaini makubwa mashabiki pamoja na benchi la ufundi. Simba inaamini kuwa sasa ni wakati wa kurejesha nguvu zao kwenye mashindano ya ndani, huku kipaumbele kikubwa kikiwa ni Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa sasa Simba ipo nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imecheza michezo saba, kukusanya pointi 16 baada ya kushinda michezo mitano, kutoka sare mmoja na kupoteza mchezo mmoja. Aidha, bado ina viporo zaidi ya sita vinavyoweza kubadilisha kabisa sura ya msimamo wa ligi endapo itapata matokeo mazuri.

Kwa upande wa KMC, wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa kwenye wakati mgumu, baada ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa ligi kwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji. KMC kwa sasa inashika mkia wa ligi ikiwa na pointi nane baada ya kucheza jumla ya michezo 14.

Licha ya tofauti ya nafasi na ubora wa vikosi hivyo viwili, timu zote zinaingia uwanjani zikiwa na kiu kubwa ya ushindi. Hata hivyo, kwa upande wa kiufundi, Simba inaonekana kuwa na ubora mkubwa zaidi ukilinganisha na KMC.

Kocha Mkuu wa Simba, Steven Barker, amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri, akisisitiza kuwa kikosi chake kinahitaji kucheza kwa umakini mkubwa, kutawala mchezo na kutumia vyema nafasi zitakazopatikana ili kuhakikisha wanapata ushindi muhimu.

The post MSIMBAZI MOTO MOTO SIMBA YAITAKA KMC KUREJEA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post BARKER AFICHUA SIRI KUONGEZA KASI BAADA YA CAF
Next Post ROBO FAINALI BADO HAI, YANGA WASHIKA MAWILI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook