Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Simba Yachechemea Ligi ya Mabingwa Baada ya Sare ya 2 – 2

  • 27
Scroll Down To Discover

Dakika 90 za mchezo mkali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC na Espérance Sportive de Tunis zimekamilika kwa sare ya mabao 2-2, katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, leo Februari 01, 2026.
Katika mchezo huo wa kukatana shoka, Simba SC walianza kwa kishindo kipindi cha kwanza baada ya kufunga mabao mawili kupitia kwa Shomari Kapombe na Yusuph Kagoma, hali iliyoipa timu hiyo matumaini makubwa ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya Afrika.

Hata hivyo, kipindi cha pili kilishuhudia Espérance de Tunis wakirudi kwa kasi na nidhamu ya hali ya juu, ambapo walifanikiwa kusawazisha mabao yote mawili na kuifanya Simba kushindwa kutimiza ndoto ya kuendelea hatua inayofuata.


Kutokana na matokeo hayo, Simba SC inachechemea kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Espérance de Tunis wakishika nafasi ya pili.

The post Simba Yachechemea Ligi ya Mabingwa Baada ya Sare ya 2 – 2 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Shabiki Ampiga Ngumi Mangungu – Video
Next Post Waziri Mkuu Asisitiza Umuhimu wa Maadili na Mshikamano Katika Jamii
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook