Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jeshi la Polisi Latoa Taarifa Kuelekea Mchezo wa Yanga na Al Ahly Kesho

  • 42
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi limetoa taarifa rasmi kuelekea mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans SC ya Tanzania na Al Ahly ya Misri, unaotarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katika taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limesema limejipanga kikamilifu kuhakikisha usalama wa wachezaji, viongozi wa timu, waamuzi pamoja na mashabiki wote watakaohudhuria mchezo huo, kuanzia kabla, wakati na baada ya mechi.

Polisi imewataka mashabiki wa soka kuzingatia sheria, taratibu na maelekezo yatakayotolewa na vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwemo kufika uwanjani mapema kwa ajili ya ukaguzi, kuepuka kubeba vitu hatarishi, na kuacha tabia zozote zinazoweza kuhatarisha amani na usalama.

Aidha, Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa halitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayekiuka sheria au kujaribu kuvuruga amani wakati wa mchezo huo mkubwa unaofuatiliwa na mashabiki wengi ndani na nje ya nchi.

The post Jeshi la Polisi Latoa Taarifa Kuelekea Mchezo wa Yanga na Al Ahly Kesho appeared first on Global Publishers.



Prev Post Serikali Yatenga Sh. Bilioni 2 Kusaidia Watengeneza Maudhui Mitandaoni
Next Post Al Ahly Wamchapa Ashour Faini Kubwa, Agoma kwenda Zanzibar
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook