Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Yatenga Sh. Bilioni 2 Kusaidia Watengeneza Maudhui Mitandaoni

  • 117
Scroll Down To Discover

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha TZS bilioni 2 itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali.

Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo.

Amebainisha kuwa, zoezi la uandikishaji wa walengwa linaanza rasmi Januari 30 hadi Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa za Miji na Majiji kupitia vitengo vya habari, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.

JESHI la POLISI LAGUSA MIOYO! LAMSAIDIA MTOTO IMANI KUTIMIZA NDOTO YAKE ya KWENDA SHULE..

The post Serikali Yatenga Sh. Bilioni 2 Kusaidia Watengeneza Maudhui Mitandaoni appeared first on Global Publishers.



Prev Post LOEMBA AICHOCHEA NDOTO YA SIMBA MAN UNITED
Next Post Jeshi la Polisi Latoa Taarifa Kuelekea Mchezo wa Yanga na Al Ahly Kesho
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook