Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rwanda Yaishtaki Uingereza kwa Kukiuka Mkataba wa Wahamiaji

  • 23
Scroll Down To Discover

Keir Starmer, Waziri Mkuu wa Uingereza.

Rwanda imeishitaki serikali ya Uingereza kwa kukiuka makubaliano ya wahamiaji Rwanda imeishtaki serikali ya Uingereza kuhusu makubaliano ya wahamiaji ambayo London imeyatelekeza yapata miaka miwili iliyopita.

Keir Starmer, Waziri Mkuu wa Uingereza ametelekeza makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya nchi mbili ambayo yalisainiwa na serikali ya wakati huo alipoingia mamlakani mwezi Julai mwaka juzi.

London iliripotiwa kuilipa Kigali pauni milioni 240 sawa na dola milioni 330.9 kabla ya makubaliano hayo kutelekezwa.

Rwanda imesema kuwa mwezi Novemba mwaka juzi, Uingereza ilitaka iachane na malipo mawili ya pauni milioni 50 ambayo Rwanda ilipaswa kulipwa mwezi Aprili 2025 na Aprili mwaka huu ikisema kuwa inafanya hivyo kwa kutarajia kusitishwa rasmi mkataba huo.

Rwanda ilieleza kuwa inaweza kukubali mipango hiyo iwapo mkataba huo utakatishwa, madhali masharti mapya ya kifedha yatajadiliwa na kukubaliwa.

Hata hivyo majadiliano kati ya Rwanda na Uingereza hatimaye hayakufanyika na kiasi hicho cha fedha kinapaswa kulipwa kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Kigali iliripoti kesi hiyo katika Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi yenye makao yake Uholanzi Novemba mwaka jana baada ya Uingereza kuweka wazi kuwa haina nia ya kufanya malipo mengine kwa mujibu wa mkataba huo.

Rwanda inamtuhumu Waziri Mkuu wa Uingereza kuwa ametangaza kwamba makubaliano hayo yamekufa na kuzikwa bila ya kuitaarifu kwanza Kigali.

NANI KUMPISHA LOEMBA SIMBA?BAJABER AU MAEMA? KOCHA AFUNGUKA-BIL.6.4 ZATUMWA AZAM KWA FEITOTO

The post Rwanda Yaishtaki Uingereza kwa Kukiuka Mkataba wa Wahamiaji appeared first on Global Publishers.



Prev Post Uwanja wa KMC Wafungiwa na TFF kwa Kukosa Vigezo
Next Post Ishi Kidigitali Kwa Kupata Taarifa Muhimu Kiganjani Mwako kwa Kutumia Simu Yako
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook