Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Uwanja wa KMC Wafungiwa na TFF kwa Kukosa Vigezo

  • 19
Scroll Down To Discover

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa KMC uliopo Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya Ligi, baada ya kubaini kuwa haukidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Kwa mujibu wa TFF, miundombinu ya uwanja huo haijakidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyoainishwa katika masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu, hali iliyopelekea kuchukuliwa kwa uamuzi huo.

Kutokana na hatua hiyo, klabu zote zinazoutumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia viwanja mbadala kwa mujibu wa Kanuni, hadi pale uwanja huo utakapofanyiwa marekebisho na kukaguliwa upya na TFF kabla ya kuruhusiwa kutumika tena.

TFF imesisitiza kuwa itaendelea kusimamia utekelezaji wa Kanuni na kuzitaka klabu zote nchini kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja ili kukidhi viwango vinavyotakiwa kwa michezo ya Ligi.

The post Uwanja wa KMC Wafungiwa na TFF kwa Kukosa Vigezo appeared first on Global Publishers.



Prev Post Wanachama 11 wa Genge la Ulaghai la Ming Wanyongwa China
Next Post Rwanda Yaishtaki Uingereza kwa Kukiuka Mkataba wa Wahamiaji
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook