Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

OUMA, TUNAKWENDA KONGO KUCHUKUA POINT TATU

  • 25
Scroll Down To Discover

KIKOSI cha wachezaji 21 cha Singida Black Stars, kimeelekea nchini Congo kucheza mechi ya nne hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Otoho d’Oyo itakayofanyika Februari 1, 2026.

Kocha wa Singida Black Stars, David Ouma amesema wameenda kuandika historia nyingine kumataifa kwa kupata pointi tatu wakiwa ugenini.

Singida Black Stars inauendea mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 nyumbani dhidi ya timu hiyo, wikiendi iliyopita zilipokutana kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar

Akizungumza na Soka la Bongo, Ouma amesema wanaenda kucheza mchezo mgumu ambao wao wameubeba kama fainali kwani umeshikilia uamuzi wa nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ambayo ameitaja kuwa itabaki katika historia bora kwa klabu yao.

“Tunakwenda tukiwa na malengo sawa kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji, hivyo mipango ipo vizuri na kila mchezaji anatambua umuhimu wa mchezo huo ambao kwetu ni kama fainali kutokana na kubeba hatma yetu. Hatutarajii mchezo rahisi, tumejiandaa kwenda kushindana na kucheza kwa kumuheshimu mpinzani wetu ambaye pia anasaka pointi tatu kama ilivyo upande wetu, mbinu bora na kujitoa kwa wachezaji ndio kutatupa nafasi ya kusonga nafasi inayofuata,”  amesema Ouma.

Ouma amesema anatambua ubora na upungufu wa wapinzani wao, hivyo amefanyia kazi katika uwanja wa mazoezi na ataendelea kusuka mbinu bora kabla ya mechi hiyo.

Wachezaji walioondoka ni Metacha Mnata, Amas Obasogie, Abdallah Said ‘Lanso’, Miraj Hassan, Kennedy Juma, Mukrim Issa, Abdulmalick Zakaria, Idd Khalid, Morice Chukwu na Khalid Aucho.Wengine ni Emmanuel Keyekeh, Idriss Diomande, Marouf Tchakei, Mtange Linda, Deus Kaseke, Lamine Jarjou, Mossi Nduwumwe, Joseph Guede, Harson Muaku, Mishamo Daudi na Elvis Rupia aliyetupia bao la ushindi mechi iliyopita.

The post OUMA, TUNAKWENDA KONGO KUCHUKUA POINT TATU appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post KUELEKEA MECHI vs AL AHLY…..KOCHA YANGA ATOA KAULI YA KISHUJAA…ILA WAAKIIFUNGWAAA🤣🤣..
Next Post UMOJA NDIO SILAHA YA SIMBA, AHMED ALLY
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook