Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Sakata la Ardhi Karagwe: Watoto wa Marehemu Wadai Kudhulumiwa Ekari 32 – Video

  • 50
Scroll Down To Discover


Sakata la familia ya marehemu Cleophace Rutaiga inayoishi Karagwe mkoani Kagera kudai kwamba baba yao mdogo kwa kushirikiana na shangazi yao wamewadhulumu watoto wa marehemu shamba lenye ukubwa wa ekari 32, linazidi kuchukua sura mpya.

Global TV imezungumza na mmoja kati ya watoto wa marehemu aliyezungumza kwa niaba ya watoto wengine wa marehemu na kueleza madai hayo ya kudhulumiwa shamba hilo walioachiwa shamba hilo na marehemu baba yao.

Global TV pia imezungumza na shangazi anayedaiwa kushirikiana na baba mdogo katika sakata hilo, ambaye ameeleza kuwa madai yanayotolewa na watoto wa marehemu, hayana ukweli kwani hawana nyaraka za kuthibitisha madai yao.

Shangazi huyo akaeleza kuwa suala hilo limewahi kupelekwa mahakamani, lakini kesi ikashindwa kuendelea kutokana na walalamikaji kukosa nyaraka muhimu za kuthibitisha madai yao.

Global TV pia ilimtafuta baba mdogo
anayetajwa kwenye sakata hilo, ambaye naye alikanusha madai hayo.

Lakini pia, Global TV ilizungumza na mdogo wa marehemu, ambaye yeye aliwaunga mkono watoto hao na kueleza kuwa ni kweli shamba hilo lilikuwa likimilikiwa na marehemu kaka yao na anawashangaa ndugu hao kwa kutaka kuwadhulumu mali yao.

The post Sakata la Ardhi Karagwe: Watoto wa Marehemu Wadai Kudhulumiwa Ekari 32 – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mbunge Musukuma ‘Azichapa’ na Mwekezaji, Serikali Yatajwa Kuchukua Hatua – Video
Next Post Serikali Yatangaza Ajira 142 NAOT kwa Fani Mbalimbali
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook