Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Marekani Yajiondoa Rasmi WHO, Trump Atekeleza Amri ya 2025

  • 37
Scroll Down To Discover

Marekani imejiondoa rasmi katika Shirika la Afya Duniani (WHO) jana, Alhamisi, Januari 22, 2026, ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump aliyoitoa siku ya kwanza ya kuingia kwake madarakani mwaka 2025.

Uamuzi huo unakuja baada ya onyo la mwaka mzima kuwa hatua hiyo inaweza kuumiza sekta ya afya nchini Marekani na duniani kote. Serikali ya Trump imesisitiza kuwa kujiondoa huko kunatokana na kile ilichokiita “kushindwa kwa usimamizi” wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa wakati wa janga la COVID-19.

Kupitia taarifa ya pamoja kutoka Idara za Afya na Mambo ya Nje za Marekani, nchi hiyo imesema itafanya kazi na WHO kwa kiwango cha chini sana ili kukamilisha mchakato wa kujiondoa. “Hatuna mipango ya kushiriki kama mtazamaji (observer), na hatuna mipango ya kujiunga tena,” alisema ofisa mwandamizi wa afya wa serikali.

Badala yake, Marekani inapanga kushirikiana moja kwa moja na nchi mbalimbali katika masuala ya ufuatiliaji wa magonjwa na vipaumbele vingine vya afya ya jamii, badala ya kupitia mashirika ya kimataifa.

Sheria ya Marekani inataka nchi hiyo kutoa taarifa ya mwaka mmoja na kulipa madeni yote yanayokadiriwa kufikia Dola milioni 260 kabla ya kujiondoa. Hata hivyo, maofisa wa Marekani wamepinga hitaji hilo la malipo.

“Wamarekani wameshalipa zaidi ya kutosha. Shirika hili limegharimu Marekani mabilioni ya dola,” amesema msemaji wa Idara ya Mambo ya Nje kupitia barua pepe.

Tayari bendera ya Marekani imeondolewa nje ya makao makuu ya WHO jijini Geneva. Hatua hii imezua hofu miongoni mwa wanadiplomasia kuwa “Bodi ya Amani” (Board of Peace) iliyoanzishwa na Trump hivi karibuni inaweza kudhoofisha mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa (UN).

Stori na Elvan Stambuli, Global Digital

The post Marekani Yajiondoa Rasmi WHO, Trump Atekeleza Amri ya 2025 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Bima Ya Afya Kwa Wote Shilingi 150,000 Kwa Kaya, Wasio Na Uwezo Kugharamiwa Na Serikali
Next Post Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Awasili Mwanza, Kuzindua na Kukagua Miradi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook