Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mume Aliyemn’gata, Kumpiga Sufuria Mkewe Apandishwa Mahakamani – Video

  • 22
Scroll Down To Discover

Hamza Omary (38), fundi Selemala na mkazi wa Luchelele, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Mkuyuni, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Januari 19, 2026, akikabiliwa na shtaka la kumshambulia mke wake katika Kesi ya Jinai namba 75/2026.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 07, 2026 katika eneo la Luchelele, Mtaa wa Kisoko, majira ya saa 3.30 usiku, ambapo alimshambulia mke wake aitwaye Anna Zacharia kwa kumpiga ngumi, kumrushia sufuria kichwani na kumng’ata mkono wa kushoto.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Mkuyuni, Mhe. Witness Ndosi, Mwendesha Mashtaka Koplo Dorothy Mauma alisema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 240 cha Sura ya 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Marejeo ya mwaka 2023.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka hilo na amepelekwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

Masharti ya dhamana yalikuwa ni kuwa na mdhamini mmoja, barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata pamoja na fungu la dhamana la ahadi kiasi cha shilingi laki moja (100,000) tu. Mhe. Witness Ndosi ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 02, 2026.

 

The post Mume Aliyemn’gata, Kumpiga Sufuria Mkewe Apandishwa Mahakamani – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post JKT Watangaza Mafunzo ya Kujitolea 2026, Usaili Kuanza Januari 26
Next Post Mkuu wa Jeshi Uganda Atishia Maisha ya Bobi Wine – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook