Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

JKT Watangaza Mafunzo ya Kujitolea 2026, Usaili Kuanza Januari 26

  • 23
Scroll Down To Discover

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ametoa wito wa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2026.

Akimwakilisha Mkuu wa JKT, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena leo tarehe 20 Januari 2026 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, amesema usaili utaanza tarehe 26 Januari 2026 kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Brigedia Jenerali Mabena ameongeza kuwa vijana watakaoteuliwa kujiunga na mafunzo ya JKT wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Februari 27, 2026 hadi Machi 04, 2026.

Katika hatua nyingine Brigedia Jenerali Mabena amefafanua kuwa JKT halitoi ajira, pia halihusiki na kuwatafutia ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mashirika mbalimbali ya Kiserikali bali hutoa mafunzo yatakayosaidia Vijana kujiajiri mara baada ya kumaliza mkataba wao na JKT.

The post JKT Watangaza Mafunzo ya Kujitolea 2026, Usaili Kuanza Januari 26 appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mzee Edwin Mtei Kuzikwa Januari 24 Arumeru Arusha
Next Post Mume Aliyemn’gata, Kumpiga Sufuria Mkewe Apandishwa Mahakamani – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook