Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

OKELLO NI MCHEZAJI WA KUAMUA MATOKEO, LULE

  • 23
Scroll Down To Discover

ALIYEKUWA  kocha wa Singida Black Stars, Mganda Mathias Lule, amemwagia sifa mchezaji Allan Okello akisema ni miongoni mwa wachezaji wenye ubora wa hali ya juu wanaoweza kuleta tofauti kubwa ndani ya uwanja.

Okello amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga akitokea katika klabu ya Vipers ya Uganda na tayaru yupo nchini kwa ajili ya kuanza majukumu yake ndani ya klabu hiyo.

Lule ambaye amewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, amesema Okello ni mchezaji mwenye ufundi mzuri (good technique) unaomwezesha kumiliki mpira kwa uhakika, kucheza kwa kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika nyakati ngumu za mchezo.

“Moja ya sifa kubwa za Okello ni uwezo wake wa kuamua matokeo ya mechi wakati wowote, hasa kutokana na akili yake ya mchezo na uwezo wa kusoma nafasi, jambo linalomfanya kuwa hatari kwa wapinzani,” amesema Lule.

Amesema  Okello ni bingwa wa mipira ya adhabu (set pieces), ana uwezo mkubwa wa kufunga au kuandaa mabao kupitia mipira ya faulo na kona, jambo linaloongeza silaha muhimu kwa timu yoyote anayochezea.

Amesisitiza  kuwa ni mchezaji wa timu, anayejali maslahi ya wenzake na anayecheza kwa kushirikiana badala ya kujitafutia sifa binafsi.

Amesema mchezaji wa aina ya Okello ni hazina  kwa kikosi chochote, kwani anaunganisha ufundi, nidhamu na mshikamano wa timu, vitu ambavyo ni msingi wa mafanikio ya muda mrefu katika soka la ushindani.

The post OKELLO NI MCHEZAJI WA KUAMUA MATOKEO, LULE appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post SIMBA YAVIZIA NYOTA WAWILI WA KIMATAIFA
Next Post KUTOKA MOROCCO HADI PEMBA KUIPA YANGA UBINGWA
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook