Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais wa zamani wa Brazil Aruhusiwa Hospitali, Arudishwa Gerezani

  • 31
Scroll Down To Discover

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro ameondoka hospitalini katika Mji Mkuu wa Brasilia, wiki moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Ngiri mara mbili, na kurudishwa Gerezani chini ya ulinzi wa Polisi wa Shirikisho kuendelea kutumikia kifungo chake cha miaka 27 jela.

Gari lilimsafirisha Bolsonaro kutoka hospitali ya DF Star hadi Makao Makuu ya Polisi, ambako anazuiliwa baada ya kukutwa na hatia ya kuongoza jaribio la Mapinduzi lililolenga kumweka ofisini.

Hospitali ilithibitisha kuwa Bolsonaro aliruhusiwa kufuatia taratibu za ziada za matibabu, ikisema upasuaji ulikuwa umekamilika bila matatizo.

Mahakama ya juu ya Brazil ilikuwa imeidhinisha kuachiliwa kwa Bolsonaro kwa muda kutoka Gerezani ili kufanyiwa operesheni hiyo.

Hata hivyo, Jaji wa Mahakama ya juu Alexandre de Moraes, ambaye alimhukumu, alikataa ombi la kuhukumiwa kifungo cha nyumbani.

AJALI ILIYOUA WATU 10 na KUJERUHI WENGINE 18 MKOANI MOROGORO -JESHI la POLISI LAANZA UCHUNGUZI MKALI

The post Rais wa zamani wa Brazil Aruhusiwa Hospitali, Arudishwa Gerezani appeared first on Global Publishers.



Prev Post Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Akagua Ujenzi wa Madrasa Ali Ba Alawi Kiluvya – Video
Next Post Fahamu Teknolojia Mpya Ndani ya Toyota Crown 2026
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook