Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Clemence Mwandambo Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Tuhuma za Kijinai – Video

  • 32
Scroll Down To Discover

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali Saint Clemence, Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni “A” jijini Mbeya, kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashifu imani za dini mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 29, 2025 na Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, mtuhumiwa alikamatwa alfajiri majira ya saa 10:00 katika maeneo ya Uzunguni.

Kwa mjibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga imeeleza kuwa Mwandambo alikuwa akitumia akaunti zake za mitandao kusambaza ujumbe unaodaiwa kupotosha na wenye kuleta mgawanyiko wa kiimani.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi unaendelea ili kukamilisha hatua zinazofuata za kisheria, endapo ushahidi utathibitisha tuhuma zinazomkabili.

The post Clemence Mwandambo Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Tuhuma za Kijinai – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Niliuanza Mwaka Nikiwa Naandamwa na Madeni Kibao na Mkwamo wa Kiuchumi
Next Post Waziri Mkuu Akagua Soko Na Kituo Cha Mabasi Bunju B – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook