Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

HERSI AIBUA DIRA YA SOKA LA AFRIKA

  • 125
Scroll Down To Discover

RAIS  wa Klabu ya Yanga  na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika (ACA), ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu ya FIFA. Hersi Said, ameendelea kuthibitisha nafasi yake katika maendeleo ya soka la Afrika baada ya kushiriki mazungumzo muhimu kwenye kipindi cha kimataifa cha @TransferRoom.

Katika mahojiano hayo,  Hersi ameeleza kwa kina dhamira ya viongozi wa soka barani Afrika katika kujenga mifumo imara itakayohakikisha vipaji vya vijana vinalindwa, vinaendelezwa na kunufaisha vilabu pamoja na wachezaji kwa muda mrefu.

Mojawapo ya mada kuu iliyojadiliwa ni maendeleo na uhifadhi wa vipaji bora barani Afrika, ambapo amesisitiza umuhimu wa vilabu kuwekeza zaidi kwenye mifumo ya ndani badala ya kuuza vipaji mapema bila mipango endelevu.

Pia amegusi  suala la kuunda njia imara kutoka shule na akademi za kufundisha mpira hadi timu za kwanza za vilabu, ameeleza kuwa mafanikio ya soka la kisasa yanategemea sana uwepo wa daraja linalowawezesha vijana kupanda hatua kwa hatua kwa misingi ya kitaalamu.

Hersi aliongeza kuwa kuwepo kwa miundombinu bora na sera sahihi kutawasaidia wachezaji vijana kupata mazingira salama ya kukua kiakili, kimwili na kiufundi kabla ya kukutana na changamoto za soka la ushindani wa juu.

Katika mjadala huo, amezungumzi pia njia za kuongeza thamani ya uhamisho wa wachezaji wa Afrika, ameeleza  kuwa maandalizi sahihi na mikataba yenye tija itaongeza heshima na mapato kwa vilabu vya bara hili.

Kwa ujumla, ushiriki wa Hersi  kwenye jukwaa la @TransferRoom umeonyesha wazi dira ya soka la Afrika linalojitegemea, lenye mifumo imara na lenye uwezo wa kufungua fursa kubwa za kimataifa kwa wachezaji na vilabu vyake.

The post HERSI AIBUA DIRA YA SOKA LA AFRIKA appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Vodacom yagawa makapu ya sikukuu kwa wateja wake Njombe
Next Post SIRI YAFICHUKA SIMBA KUKOSA MATOKEO, MAGORI
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook