Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

WADAU MADALE WAHIMIZWA KUJIUNGA NA SACCOS KWA USTAWI WA KIUCHUMI

  • 117
Scroll Down To Discover

Na John Bukuku – Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Madale Wadau Group, Bw. Stephen Kazimoto, ametoa ripoti maalum ikionyesha faida na umuhimu wa wanakikundi kujiunga na SACCOS kama njia ya kujenga uthabiti wa kifedha na kuongeza nguvu ya maendeleo ya kiuchumi kwa pamoja.

Amesema SACCOS ni chombo muhimu cha kuweka akiba na upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu, hivyo wanachama wana nafasi kubwa ya kupanua biashara, kukabiliana na dharura na kuwekeza kwenye shughuli za kijamii kama elimu na ujenzi.

Katika ripoti yake, Kazimoto amefafanua kuwa kupitia SACCOS wanachama hujengewa utamaduni wa kuweka akiba mara kwa mara, jambo ambalo linawaongezea hisa, nguvu ya kukopa na nidhamu katika matumizi ya fedha. Ameongeza kuwa mfumo huu huwasaidia kutimiza malengo yao ya kifedha kwa urahisi zaidi.

Aidha, ameeleza kuwa wanachama wa SACCOS hupata gawio (dividends) kila mwisho wa mwaka kulingana na kiwango cha hisa walizowekeza, kitendo kinachowatia moyo wengi kuongeza akiba zao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama.

Bw. Kazimoto pia amebainisha kuwa SACCOS nyingi hutumia mifumo ya bima ya mikopo, hatua ambayo inalinda mali na maslahi ya wanachama, hivyo kupunguza hatari ya kupoteza fedha endapo changamoto zitajitokeza.

Akizungumzia upande wa kujengewa uwezo, amesema wanachama hupata mafunzo ya ujasiriamali, uongozi, usimamizi wa fedha pamoja na mbinu za kilimo na biashara, jambo linaloongeza maarifa na uwezo wa kujitegemea kiuchumi.

“Mara nyingi tunashuhudia faida ya ushirika kupitia msaada wa kifedha na kijamii pale mwanachama anapopatwa na changamoto. Ndio maana tunasisitiza kuwa nguvu ya pamoja ni msingi wa ustawi wetu,” amesema Kazimoto.

Ripoti hiyo pia imeonyesha hali ya makusanyo ya kikundi ikiwa ni Shilingi 12,370,000/= zikiwemo Shilingi 2,750,000/= za kiingilio, Shilingi 5,100,000/= za hisa na Shilingi 4,529,000/= za ada.

Akihitimisha, Mwenyekiti huyo amesema kujiunga na SACCOS ni hatua madhubuti kwa kikundi chochote kinacholenga kujijenga kiuchumi kwani kunatoa fursa ya mikopo nafuu, uwekezaji wa pamoja, usalama wa fedha na mtandao mpana wa ushirikiano. Amehimiza wanachama wa Madale Wadau Group kuendelea kujiunga ili kuongeza uwezo wa kufikia malengo ya pamoja na binafsi.



Prev Post Fahamu Maporomoko ya Maji Yanayopatikana Tanzania, Miji Inateseka Kwa Maji – Video
Next Post PRINCE DUBE ATIKISA DODOMA KIVINGINE
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook