Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

RAIS SAMIA AKUTANA NA NAIBU MWENYEKITI BARAZA LA BIASHARA JUMUIYA YA MADOLA (CWEIC)

  • 70
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Mhe. Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025. 

Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira. 

Aidha, Lord Swire ameomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola.



Prev Post Petroli yashuka bei. Hizi ni bei za mikoa yote kwa Desemba 2025
Next Post BAADA YA KUPIGWA MECHI 2 CAF….IBENGE AWAPA UKWELI MCHUNGU AZAM FC…
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook