Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Simba Yasitisha Mkataba na Meneja Mkuu Dimitar Pantev, Matola Kuiongoza Kwa Muda

  • 56
Scroll Down To Discover

Uongozi wa Klabu ya Simba SC umetangaza rasmi kuachana na Meneja Mkuu, Dimitar Pantev, baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha mkataba. Aidha, wasaidizi wake wawili nao wameondoka pamoja naye katika hatua hiyo ya mabadiliko ya kiufundi.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, majukumu ya kuisimamia timu kwa sasa yamekabidhiwa kwa Kocha Selemani Matola, ambaye atakaimu nafasi hiyo wakati mchakato wa kumpata kocha mpya ukiendelea.

Mabadiliko haya yanakuja kipindi ambacho Simba inaendelea na maandalizi ya michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano ya kimataifa, huku ikilenga kurekebisha mwenendo na kuongeza ushindani katika hatua zilizosalia za msimu.

The post Simba Yasitisha Mkataba na Meneja Mkuu Dimitar Pantev, Matola Kuiongoza Kwa Muda appeared first on Global Publishers.



Prev Post Je, Tume ya Oktoba 29 itajibu maswali magumu kuhusu vurugu za uchaguzi? Katika Dira ya Dunia TV
Next Post Rais Samia: Matukio ya Oktoba 29, Yalipangwa kwa Lengo la Kuangusha Dola – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook