Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi dhidi ya Viongozi wa CHADEMA – Video

  • 59
Scroll Down To Discover

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kesi ya kudharau amri ya Mahakama iliyokuwa imefunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche yametupiliwa mbali

Akisoma uamuzi wa Mahakama hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa kwa hati ya dharura amesema, Mahakama imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima.Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahakamani hapo nje ya muda

Jaji Mbagwa amesema kesi ya msingi namba 8960/2025 iliyoko chini ya Jaji Hamidu Mwanga ndio iliyokuwa msingi wa kesi iliyokuwa mbele yake, na kwamba amri ya Mahakama kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA ilitolewa na Mahakama Juni 10.2025

Aidha, Jaji Mbagwa ameendelea kufafanua kuwa kesi ya kudharau amri ya Mahakama ililetwa Mahakamani hapo Oktoba 03 mwaka huu takribani siku 106 jambo ambalo halikubaliki kisheria, Sheria inataka maombi ya aina hiyo yaletwe ndani ya siku 60.

The post Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi dhidi ya Viongozi wa CHADEMA – Video appeared first on Global Publishers.



Prev Post Waziri Kombo Apokea Magari Mawili kutoka Qatar
Next Post Dkt. Migiro Aongoza Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook