Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Urusi na Ukraine Zashambuliana Usiku: Watu Wafariki, Majengo Yaharibiwa, Bei za Mafuta Yapanda

  • 8
Scroll Down To Discover

Urusi na Ukraine zimeshambuliana usiku wa kuamkia leo kwa ndege za droni na makombora huku mashambulizi hayo ya kila upande yakisababisha vifo na uharibifu wa majengo.

Shambulizi la Urusi la usiku wa kuamkia leo zaidi likiulenga mji mkuu wa Kiev, limewaua watu wanne na kuharibu majengo kote mjini humo, kulingana na mamlaka za Ukraine. Rais Volodmyr Zelensky amesema “hilo lilikuwa shambulio lililopangwa kwa makusudi lililolenga kusababisha madhara makubwa kwa watu na miundombinu ya kiraia.” Ameongeza kuwa Urusi imerusha droni zipatazo 430 na makombora 18.

Huduma ya dharura ya Ukraine imewaokoa mamia ya watu kutoka katika majengo yaliyoshika moto na kuharibiwa katika shambulizi hilo wakati polisi wakisema nyumba zipatazo 30 za maakazi ya watu zimeharibiwa katika wilaya tisa.

Kwa upande mwingine, Ukraine nayo imefanya shambulizi la droni mapema leo ijumaa na kuharibu meli iliyokuwa imetia nang’a, majengo ya makaazi na ghala la mafuta katika mji wa bandari nyeusi wa Urusi wa Novorossiysk na kuwajeruhi wafanyakazi watatu.

Bandari hiyo ni njia muhimu kwa usafirishaji wa mafuta ya Urusi. Bei za mafuta duniani zimepanda kwa asilimia 2 kutokana hofu ya usambazaji baada ya shambulio hilo.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov akizungumza na waandishi wa habari jana alisema Urusi bado inataka amani. “Urusi inataka amani. Urusi iko tayari kusuluhisha suala la Ukraine kupitia njia za kisiasa na kidiplomasia.

Lakini kukosekana kwa fursa kama hiyo, huku serikali ya Kiev ikifunga mlango wake, tutaendelea na operesheni maalum ya kijeshi. Kipaumbele chetu kikuu ni kuhakikisha masilahi yetu, usalama kwa vizazi vijavyo na kutimiza majukumu yaliyo mbele yetu.”

Stori na Elvan Stambuli – Global Publishers



Prev Post Waziri Mkuu Afanya Ziara Ya Kushtukiza Hospitali Ya Mkoa Wa Dodoma – Video
Next Post Hii hapa Hotuba ya Rais Dkt. Samia Akifungua Bunge la 13, Novemba 14, 2025 – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook