Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia: Vyombo vya habari vitapewa nafasi na leseni kwa haki

  • 10
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itaendelea kulinda na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari ili wananchi wapate taarifa sahihi, kwa wakati na kutoka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza Ijumaa, Novemba 14, 2025 jijini Dodoma wakati wa kulifungua Bunge la 13, Rais Samia amesema uhuru wa vyombo vya habari ni msingi wa uwazi, uwajibikaji na kujenga taifa lenye uelewa mpana kuhusu masuala yanayolihusu.

“Mheshimiwa Spika, tutaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari ili Watanzania wapate haki ya kupata taarifa za ndani na nje ya nchi. Tutaendelea kutoa leseni kwa vyombo vya habari na kuulinda uhuru wa kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za nchi,” amesema.

Rais Samia amesema serikali itaendelea kuimarisha vitengo vya habari serikalini ili viwe na uwezo wa kutoa taarifa kwa weledi, kwa uwazi na kwa wakati. Aidha, amebainisha kuwa serikali itaendelea kutambua mchango wa wanahabari kupitia Tuzo ya Samia Kalamu Awards, ambayo inalenga kuhamasisha uandishi wa habari za maendeleo.

“Tutaimarisha vitengo vya habari vya serikali ili viweze kutoa habari kwa weledi na kwa wakati. Aidha, tutaendelea kutambua waandishi wa habari za maendeleo nchini kupitia tuzo ya Samia Kalamu Awards,” amesisitiza.

Akiendelea kuelezea mwelekeo wa utamaduni na sanaa, Rais Samia amesema maendeleo ya nchi yanaakisiwa pia na ustaarabu na utamaduni wake. Amesema katika dunia ya sasa, utamaduni ni bidhaa na ni uchumi, hivyo serikali itawekeza katika kukuza thamani ya Kiswahili na sanaa za filamu nchini.



Prev Post Hii hapa Hotuba ya Rais Dkt. Samia Akifungua Bunge la 13, Novemba 14, 2025 – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook