Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

DR Congo: Askari Mwenye Umri wa Miaka 102 Bado Anahudumu Baada ya Miaka 78

  • 49
Scroll Down To Discover

Mwanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sajenti Meja wa Kwanza Luhembwe Alfani, amevutia hisia za wengi baada ya kutimiza miaka 102 huku akiendelea kutumikia jeshi akiwa bado hai kazini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu wa Ulinzi wa Kitaifa, Guy Kabombo Muadiamvita, Alfani amehudumu katika jeshi la FARDC kwa miaka 78 ya uaminifu na kujitolea.

“Miaka 78 ya uaminifu kwa taifa la Kongo katika safu za FARDC Sajenti Meja Alfani, bado yuko kazini chini ya bendera ya taifa,” aliandika Muadiamvita kwenye mitandao ya kijamii.

Afisa huyo wa ulinzi aliahidi kuwa Serikali itampatia Alfani tuzo maalum kwa mchango wake mkubwa na wa kihistoria katika kulitumikia taifa hilo.

Hadi sasa haijabainika kwa nini hajastaafu, lakini wengi wamemsifu kama nembo ya nidhamu, uaminifu na uzalendo wa kweli ndani ya jeshi la Kongo.

SPIKA ZUNGU AMFOKEA BABA LEVO – “HILO SIYO JINA LAKO – RUDIA TENA KUAPA kwa JINA LAKO”…..



Prev Post Wanawake Wengi Wapo Jela India Kisa Unga
Next Post Bunge Kumthibitisha Waziri Mkuu na Kumchagua Naibu Spika Kesho
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook