Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Serikali Kujenga Miundombinu ya Kisasa

  • 23
Scroll Down To Discover

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema Serikali zote mbili chini ya  Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Ali Mwinyi zimedhamiria kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Michezo kwa kujenga miundombinu ya kisasa ya michezo mbalimbali pamoja na kufundisha wataalamu wa michezo ili kuibua vipaji na kuinua viwango vya michezo Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Viwanja vya Michezo vya Priz katika eneo la Kilimani Unguja Zanzibar leo tarehe 24 Aprili 2025 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.

Amesema jiwe la msingi la ujenzi wa viwanja hivyo vya michezo ni mwendelezo wa uwekezaji katika sekta ya michezo ambayo ni miongoni mwa sekta za kimkakati zinazokua kwa kasi na inayotarajiwa kutoa hamasa na kuvutia mashindano ya michezo mbalimbali katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Amesema Serikali kupitia Wizara zinazohusika na Michezo itaendelea kuhamasisha jamii kushiriki katika michezo yote ikiwemo michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete riadha, bao, drafti, karata, mieleka, mchezo wa ngombe, mbio za baskeli na mbio za ngalawa. Makamu wa Rais ameongeza kwamba ni dhamira ya Serikali kuendelea kutoa fursa kwa watoto, vijana, wanafunzi, wanawake na watu wenye ulemavu kushiriki katika michezo mbalimbali kwenye mazingira rafiki na yenye usalama zaidi.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema viwanja vinavyojengwa hivi sasa vimezingatia kwa kiasi kikubwa utatuzi wa changamoto mbalimbali ambazo zinazoyakumba makundi maalum katika kushiriki michezo kama vile udhalilishaji, umbali mrefu wa kufuata viwanja na miundombinu isiyowezeshi kwa wachezaji wenye mahitaji maalumu na wanawake.

Makamu wa Rais amesisitiza maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano yaende sambamba na shughuli ya kuhifadhi mazingira, kama upandaji miti katika maeneo ya viwanja vya michezo, maeneo ya kupumzikia na maeneo mengine pamoja na kuhimiza usafi wa mazingira, ikiwemo kutumia nishati safi ya kupikia.



Prev Post Balozi Nchimbi Kwa Nyerere, Akabidhiwa ’Kifimbo’ Kwa Kukubalika
Next Post Jeneza la Papa Francis kufunikwa kesho Ijumaa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook