Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Jeneza la Papa Francis kufunikwa kesho Ijumaa

  • 29
Scroll Down To Discover


Ibada ya kufunga jeneza la Hayati Papa Francis inatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa usiku Aprili 25, 2025, katika Basilika ya Mtakatifu Petro, Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Jumatano Aprili 23, 2025 na Mshereheshaji wa Nyumba ya Kipapa Jumatano, jeneza hilo litafungwa saa mbili kamili usiku kwa saa za Ulaya, sawa na saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Ibada hiyo itaongozwa na Mwadhama Kardinali, Kevin Joseph Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma, kwa mujibu wa kanuni rasmi za mazishi ya Papa wa Roma (Ordo Exsequiarum Romani Pontificis nn. 66-81).

Mshereheshaji wa maadhimisho ya Kipapa, Askofu Mkuu Diego Ravelli, amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba ibada hiyo ni sehemu ya mfululizo wa taratibu za heshima za mwisho kwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani.



Prev Post Makamu wa Rais Dkt. Mpango: Serikali Kujenga Miundombinu ya Kisasa
Next Post Tundu Lissu Agomea Kesi ya Mtandaoni, uamuzi Aprili 28
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook