Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mchakato wa Kumchagua Papa Mpya Waanza Vatican, Adaiwa Kutoka Afrika au Asia

  • 33
Scroll Down To Discover

Kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis kimeilazimisha Vatican kuitisha kikao cha kihistoria cha kumchagua mrithi wake; lakini swali linaloulizwa ni kwamba, je, papa ajaye atatoka Afrika au Asia?

Ni baada ya Vaticani kutangaza jana kwamba Papa Francis, ambaye jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio, amefariki dunia baada ya kulazwa hospitalini kwa ugonjwa wa kupumua wa nimonia ya pande zote mbili (bilateral pneumonia). Alichukua wadhifa huo wa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki mwaka 2013 akiwa wa kwanza asiye Mzungu wa Ulaya, tangu karne ya 8.

Kardinali Mario Grech

Uchaguzi wa mrithi wake utafanywa na Jumuiya ya Makardinali, inayoundwa na makadinali 138 walio chini ya umri wa miaka 80 (110 walioteuliwa na Francis). Mchakato huo unaoanza wiki mbili hadi tatu baada ya kifo cha papa unahusisha upigaji kura wa siri katika Kanisa la Sistine Chapel huko Vatican.

Mgombea lazima awe mwanamume Mkatoliki aliyebatizwa, lakini kwa kawaida huchaguliwa kutoka miongoni mwa makadinali. Theluthi mbili za kura zinahitajika kwa ajili ya kuchaguliwa kuwa papa, na moshi mweupe kutoka kwenye bomba la moshi la Sistine Chapel huwa ni ishara ya mafanikio ya mchakato huo.

Kardinali Luis Antonio Tagle

Kuwepo makadinali wa mataifa tofauti walioteuliwa na Papa Francis kumeibua uwezekano wa kuchaguliwa papa kutoka Afrika au Asia, ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada ya karne nyingi.

Kutoka Afrika, Peter Turkson wa Ghana, aliyehudumu katika Baraza la Kipapa la Haki na Amani, na Fridolin Ambongo Besungu wa Kongo, kwa sababu ya juhudi zake za kuimarisha amani, wanatambuliwa kuwa machaguo yenye nafasi nzuri zaidi kuchaguliwa.

Kutoka Asia, anatajwa Luis Antonio Tagle wa Ufilipino.Swali kuu, Je papa ajaye atatoka Afrika au Asia? Tusubiri tuone.

Kardinali Fridolin Ambongo Besungu
Kardinali Peter Erdo
Kardinali Willem Jacobus Eijk

 

Stori: Elvan Stambuli | GPL



Prev Post Mchakato wa Kumchagua Papa Mpya Waanza Vatican, Adaiwa Kutoka Afrika au Asia
Next Post D Voice Akutana Na Hitmaker Wa ‘Ginger’ L.A.X Nigeria.
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook