Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wananchi Ludewa Watakiwa Kuwa Mabalozi Katika Uhifadhi wa Misitu

  • 18
Scroll Down To Discover


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amewataka wananchi Ludewa kuwa mabalozi katika uhifadhi wa misitu na mazingira na kudhibiti moto kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.

Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua semina ya kujengeana uwezo kuhusu uhifadhi wa misitu na mazingira na njia za kuzuia na kudhibiti moto iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Ludewa, Mkoani Njombe leo Aprili 18,2025.

“Misitu yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uchomaji moto holela na ukataji wa miti hovyo kwa matumizi mbalimbali ya kibinadamu kama vile uandaaji wa mashamba, kuchoma mkaa na kuni kwa ajili ya kupikia hivyo ninyi mnaopata mafunzo haya mkawe mabalozi wa kupeleka elimu mtakayoipokea hapa kwa wananchi mnaowaongoza ili kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki katika shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira” amesisitiza Mhe. Chana .


Amefafanua kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo, Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za utatuzi ikiwemo kufanya doria za mara kwa mara, kutoa elimu ya kuzuia uchomaji wa moto na kugawa miche ya miti na mizinga ya nyuki katika maeneo mbalimbali yanayozungukwa na misitu.

Mhe. Chana ametoa rai kwa Halmashauri za Wilaya kuwa na utaratibu wa kujadili mara kwa mara masuala ya uhifadhi wa misitu, utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla kwani kwa kufanya hivyo ni kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasan, katika kuhifadhi mazingira kwa kutokata miti na kutumia nishati safi ya kupikia.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas amesema kuwa mafunzo hayo yataongeza tija katika utunzaji wa mazingira na misitu hasa kiuchumi na kwamba halmashauri itatoa ushirikiano kuhakikisha malengo ya uhifadhi yanafikiwa.

Semina hiyo imehudhuriwa na Viongozi wa Chama na Serikali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Waheshimiwa Madiwani wa Kata za Wilaya ya Ludewa, Wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Wadau mbalimbali wa uhifadhi kutoka kata za wilaya ya Ludewa.

Na Happiness Shayo-Ludewa



Prev Post MAGAZETI ya Leo Jumamosi 19 April 2025
Next Post Mazishi ya Aliyekuwa Msanii wa Filamu, Carina Katika Makaburi ya Kisutu (Picha +Video)
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook