Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mstaafu Kikwete Awasilisha Ujumbe Maalum Kwa Waziri wa Nchi ya Guinea ya Ikweta

  • 31
Scroll Down To Discover

Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasilisha Ujumbe Maalum ambao ulipokewa na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Guinea ya Ikweta, Mhe. Simeon Oyono Esono Angue, kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo, Mhe. Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Uwasilishaji wa ujumbe huo ulifanyika katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Malabo tarehe 13 Aprili 2025.

Katika tukio hilo, Mhe. Kikwete pia alitoa salamu za Rais Samia, akisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano, mshikamano, na umoja ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto zinazokabili Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.



Prev Post MAGAZETI ya Leo Jumatatu 14 April 2025
Next Post Kiongozi wa Mapinduzi Gabon Jenerali Nguema Ashinda Uchaguzi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook