MAGAZETI ya Leo Jumatatu 14 April 2025
Tanzania iko mbioni kuacha kuagiza vilipuzi na baruti kutoka nje ya nchi. Kila mwaka Tanzania inaagiza vilipuzi milioni 10 na tani 26,000 za baruti kutoka nje.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema nchi iko mbioni kuachana na uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi kutokana na uzalishwaji wa zana hizo muhimu katika sekta ya madini.
Amesema Kiwanda cha Solar Nitrochemicals Limited kilichozinduliwa Jumapili, Aprili 13, 2025 kitakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa hiyo zaidi ya mahitaji.
Akizindua kiwanda hicho kilichogharimu Sh19 bilioni, Waziri Mavunde amesema kitazalisha tani 22,000 za baruti na vilipuzi milioni 15 kwa mwaka.
“Tunaelekea kuacha kuagiza vilipuzi na baruti kutoka nje,” amesema Mavunde wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo eneo la Visegese, Kisarawe mkoani Pwani.
Amesema kiwanda hicho ni cha kwanza kuzalisha kiwango kikubwa cha baruti na vilipuzi nchini na kwamba, uzalishaji huo utaongeza pato la Taifa kupitia sekta ya madini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!