Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Davido Apewa Siku 21 Kujibu Kesi Ya Kuiba Wimbo.

  • 25
Scroll Down To Discover

Kwa Mujibu Wa Ripoti Mbalimbali, Mahakama ya Manhattan Nchini Marekani, imempa #Davido siku 21 kujibu kesi ya madai ya kuiba wimbo. Wasanii wanne kutoka Nigeria “Martins Chukwuka, Abel Umaru, Kelvin Campbell, na David Ohioghena” wanamtuhumu Davido kuiba wimbo wao Uitwao “Work” Wa 2022 na kuutumia kutengeneza Ngoma Yake Ya “Strawberry on Ice” Alioutoa 2024.

Wasanii Hao Wanadai Kuwa Walituma wimbo Huo kwa Davido kwa ajili ya collabo Januari 2022, lakini badala yake alimpa Emmerson (msanii wa Sierra Leone) Na Kisha Kuu-sample bila ruhusa. Madai yanaonyesha Davido alikubali kulipa $45,000 (Tsh Milioni 120/=) na kugawana mirabaha, lakini hakutimiza makubaliano hayo. Hivyo wasanii hao wanadai fidia ya $150,000 (Tsh Milioni 400/=) pamoja na haki zao za umiliki wa wimbo.

Wimbo wa ‘Work’ ambao unadaiwa kuwa Davido Ameu-Sample katika Ngoma Yake Ya ‘Strawberry on Ice’ bado haujapatikana Kwenye Majukwaa Ya Kusikilizwa Muziki, Kwani Hata baada ya kusambaa kwa taarifa za kesi Hii, hakuna kipande cha wimbo huo kilichowekwa kwenye Digital Platforms Za muziki kama YouTube, SoundCloud, au Apple Music. Hii inaweza kuwa wimbo huo haujatoka rasmi au Ulitumika kama demo tu Kabla ya kutokea kwa mzozo huu Au Uliwekwa Private.

The post Davido Apewa Siku 21 Kujibu Kesi Ya Kuiba Wimbo. appeared first on Wasafi Media.



Prev Post Keri Hilson Adai Alilazimishwa Kum-Diss Beyonce.
Next Post Makalla Avalia Njuga Changamoto za Barabara,Wanyamapori na Umeme Liwale
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook