Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Keri Hilson Adai Alilazimishwa Kum-Diss Beyonce.

  • 22
Scroll Down To Discover

Mwanamuziki #KeriHilson Kwenye Mahojiano Na @breakfastclubam amefunguka kuhusu Kitu Anachokijutia. Keri Amesema kuwa ule wimbo wa “Turnin’ Me On (Remix)” ambao ulikuwa na maneno ya kumdiss #Beyoncé, Haukuandikwa Na yeye, bali alilazimishwa kuuimba.

Keri Anasema aliandika version yake mwenyewe ya wimbo huo ambayo haikutolewa, lakini version nyingine ilitolewa ambayo iliandikwa na mwandishi mwingine. Keri anadai kuwa wakati huo alikuwa amesainiwa kwa #PolowDaDon, ambaye ndiye aliyemlazimisha aimbe diss hiyo. Pia aliahidiwa kuwa wimbo huo hautatolewa, lakini baadaye Ulivujishwa Mtandaoni.

“Ule Wimbo Kiukweli Sikuuandika Mimi, Yale Sio Mashairi Yangu” – Keri Hilson

Hata Hivyo Mwandishi Wa Remix Ya Wimbo Huo ‘Ester Dean’ Ameibuka Na Kuthibitisha Kuwa Yeye Ndiye Aliyeandikwa Remix Hiyo Na Sio Keri Hilson

Mwandishi ‘Ester Dean’ Alivyoibuka Na Kuthibitisha Kuwa Ndio Aliyemwandikia Keri Hilson Diss Track Ya Beyonce

The post Keri Hilson Adai Alilazimishwa Kum-Diss Beyonce. appeared first on Wasafi Media.



Prev Post Songwe, Njombe, Mbeya na Ruvuma Kukosa Umeme Kesho
Next Post Davido Apewa Siku 21 Kujibu Kesi Ya Kuiba Wimbo.
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook