Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Rais Samia Akutana na Mmiliki wa Man United Wafanya Mazungumzo Ikulu Dar

  • 20
Scroll Down To Discover

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Aprili, 2025.

Katika mazungumzo yao Rais Dkt. Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibiti muingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza Sir Jim Ratcliffe

Kupitia Taasisi yake ya Six Rivers, Sir Jim Ratcliffe amebainisha kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhi ya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo.



Prev Post Balozi Nchimbi Akutana Na Mwenyekiti Wa Wabunge Wa CCM, Spika Wa Bunge
Next Post Cheza Book of Eskimo Kasino Bora ya Meridianbet
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook