Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Dkt. Samia Ahimiza Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mugumu Serengeti Kuendeleza Utalii – Video

  • 10
Scroll Down To Discover

Mara/Simiyu, Oktoba 10, 2025 — Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kujenga Uwanja wa Ndege Mugumu Serengeti kama sehemu ya adhma ya CCM ya kufikisha idadi ya watalii milioni nane wanaoitembelea Tanzania kwa mwaka kufikia mwaka 2030.

Akihutubia wananchi wakati wa mikutano ya kampeni mkoani Mara na kurejea Simiyu, Dkt. Samia pia ameahidi kuendelea kutangaza vivutio na kukuza utalii wa Tanzania, akiitaja Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kama nguzo muhimu ya utalii kutokana na mafanikio yake ya kimataifa, ikichukua tuozo bora mara tatu mfululizo.

“Mji huu wa Serengeti una umuhimu mkubwa na fursa za uwekezaji wa hoteli za utalii, kwani upo katikati ya maeneo yaliyohifadhiwa kwa wageni wanaotoka Sirari na Seronera kwenda Kogatende, kaskazini mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambapo pia kuna utalii wa nyumbu wanaohama kwenye ikolojia ya Serengeti,” alisema Dkt. Samia.

Aidha, Dkt. Samia ameahidi kuongeza kasi katika uhudumu wa jamii, akizingatia mahitaji muhimu ya wananchi ikiwemo: Afya, Elimu, Maji, Kilimo, Miundombinu ya barabara, Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi

Dkt. Samia amehitimisha mikutano yake ya kampeni kwa kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, huku akisisitiza umuhimu wa maendeleo endelevu ya utalii na ustawi wa wananchi.



Prev Post Kikwete: Sijafa Mimi Mzima Sina Ninapougua, Wanaoniobea Mabaya Watatangulia Wao – Video
Next Post Askofu Dallu Atangaza Kutoweka kwa Padri Camillus Nikata, Waomba Msaada wa Polisi – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook